Thursday, 18 August 2016

USIWE TU NA BORA ENEO.KUWA NA ENEO BORA LA UFUGAJI SAMAKI

Kumekuwa na na tatizo kubwa sana ambalo limewakuta watu wanaotaka kuanza mradi ya ufugaji wa samaki,ardhi kitu kikubwa na muhimu sana katika mradi wa ufugaji wa samaki,lakini Aques ltd inakupa angalizo usiwe tu na eneo ilimradi bali kuwa na eneo bora lenye sifa zote za ufugaji samaki.
Kuna sifa nyingi sana hususani za kitaalamu lakini zipo nyingine ambazo haziitaji kabisa utaalamu,moja ya sababu huyo ni uwepo wa ardhi inayotuamisha maji kwa muda mrefu kwa kipindi kisichopungua miezi nane kwa kina kisichopungua mita moja.
Sifa nyingine ni uwepo wa maji ya kutosha hii itakupunguzia gharama zisizo za lazima ikiwemo matumizi ya mashine ya maji ama wakati utahitaji uchimbe.
Ni vyema kutafuta eneo lenye mfinyanzi husaidia kuanza mradi wako unafuu kuliko kupata eneo ambalo utalazimika kujenga kwa malighafi nyingine ambazo katika uhalisi inaongeza gharama.
moja ya eneo la mfugaji samaki lenye sifa nzuri ikiwemo pembeni imepita mfereji wa maji hivyo kuingiza maji kirahisi katika bwawa lake.


Muonekano halisi wa bwawa la kutumia udongo wa mfinyanzi ambalo hujengwa kwa bei nafuu hivyo kupata faida kubwa Zaidi.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa