Thursday, 18 August 2016

VIJANA KWA PAMOJA TUKIAMUA KUUNGANA TUNAWEZA KUJIAJIRI KUIPITIA UFUGAJI SAMAKI.

Wahenga husema umoja ni nguvu na utengano ni udhaifu.Ni kweli kabisa,kila mtu atakubaliana na msemo huu.Kwa sasa katika nafasi ya kujikwamua kiuchumi na utafutaji wa ajira,vijana kwa sasa hatuna budi kujiwekea mipango ya dhati ya kujikwamua kiuchumi.
Umoja ni jambo zuri sana katika kupata mafanikio kwa walio waliyapata kwa kuungana kufanya kuwa nguvu ya pamoja.
Mkuregenzi mkuu wa kampuni ya AQUES LTD bwana Emmanuel Godfrey walitembelea mradi ya ufugaji wa samaki ulipo pugu kinyamwezi na kukuta shughuli mbalimbali za miradi ya samaki zikiendelea,alikuta vijana mbalimbali wakiwemo wanafunzi kutoka vyuo vikuu kikiwemo chuo kikuu cha Dar es salaam na chuo kikuu cha kilimo SUA,kiongozi huyo alipata nafasi ya kuwaeleza fulsa zilizopo katika miradi ya ufugaji wa samaki hivyo wasisite kabisa kujiajiri wenyewe kwa kuunda vikundi vyao na kwa kuwa wenye ni wataalamu wataweza kufanikiwa Zaidi huku akitolea mfano kwa nchi kadhaa alizotembelea ikiwemo nchi ya Uganda na Misri moja ya nchi ambazo zimepiga hatua kubwa sana za kimaendeleo kupitia ufugaji wa samaki. 
Mkuregenzi wa AQUES LTD akiongea wanafunzi katika kituo cha ufugaji samaki pugu kinyamwezi.


 Mkuregenzi wa AQUES LTD akipata picha ya pamoja na vijana ambao wanajishighulisha na miradi ya ufugaji samaki.
Moja ya mabwawa makubwa kabisa ya kufugia samaki.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa