Friday, 16 September 2016

FAHAMU USICHOKIJUA KUHUSU UHUSIANO WA MBUYU NA SAMAKI.


Mungu ameumba miti na mimea kwa ajili ya binadamu. Kila mti au mmea una makusudio yake. Mbuyu ni miongoni mwa miti yenye faida nyingi na maajabu mengi. Vitu vyote vilivyomo kwenye mbuyu vinatumika kama chakula au dawa kwa faida ya binadamu na viumbe vingine.
Unga wa ubuyu unaelezwa kuwa na vitamini na madini mengi kuliko matunda mengine yoyote unayoyajuwa.
1. Inaelezwa kuwa
 unga wa ubuyu una vitamini C nyingi mara 6 zaidi ya ile inayopatikana katika machungwa.
2.
 Ubuyu una kiwango kingi cha madini ya Kashiamu (Calcium) mara 2 zaidi ya maziwa ya ng’ombe, pia madini mengine yapatikanayo katika ubuyu ni pamoja na madini ya Chuma, Magnesiamu na Potasiamu ambayo ni mara 6 zaidi ya ile potasiamu ipatikanayo katika ndizi!
3. Husaidia kujenga neva za fahamu mwilini
4. Ina virutubisho vya kulinda mwili
5. Ubuyu una vitamini B3 na B2 ambayo ni mhimu katika
 kuondoa sumu mwilini na umeng’enyaji wa madini ya chuma, kimsingi vyakula vyenye afyazaidi kwa ajili ya mwili ya binadamu huwa pia huwa na vitamin B2.
6. Unaongeza
 kinga ya mwili sababu ya kuwa na kiasi kingi cha vitamini C
7. Huongeza nuru ya macho
8. Husaidia kuzuia kuharisha na kutapika
9. Ina magnesiam ambayo husaidia kujenga mifupa na meno
10. Husaidia wenye presha ya kushuka na wenye matatizo ya
 figo
hizo ndizo faida za unga wa ubuyu na virutubisho vilivyomo ndani yake,hapa hakuna mtaalam wa mimea hapana lakini kama wadau wa samaki tunaangaliaje faida ya mti huu na tunda lake katika mabadiliko ya ukuzaji wa samaki kupunguza gharama za baadhi virutubisho ambavyo kwa wafugaji wengi vimeonekana ni gharama kubwa sana kwao.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa