Friday, 16 September 2016

MKURUGENZI WA AQUES LTD TANZANIA NZINGULA M .ZACHARIA ASISITIZA VIJANA KUJIAJIRI.

Wakati vijana wengi sasaivi wakiwa wamemaliza vyuo vya katika ngazi za astashahada ,stashada na shahada katika fani mbalimbali,kiongozi wa kampuni ya AQUES LTD TANZANIA bwana Nzingula M.Zacharia amewataka wahitimu hao kwa pamoja kuunganisha taaluma zao na kujiajiri wenyewe bila kutegemea serikali au kutoka kwa watu binafsi.
Taasisi mbalimbali zipo ambazo zimeweka mikopo ya masharti nafuu kwa ajiri ya kuruhusu watu hususani vijana ambao ndio nguvu kazi ya taifa kujiajiri wenye kupitia taaluma zao wenyewe,akatolea mfano mtu umesomea mambo ya ufugaji wa samaki na unaamini kabisa ufugaji samaki unalipa unashindwa nini kuthubutu kutafuta wadau wakakuonesha njia nzuri ya wewe kuweza kufanikisha ndoto yako kuliko kuwa tegemezi kwa familia jambo ambalo kwa upande wa pili kwa taifa umelipa mzigo wa kukuhudumia.
Kiongozi huyo pia alichukua fulsa hiyo kuwapongeza wahitimu kutoka wakala wa mafunzo ya uvuvi FETA na kuwaomba waangalie fulsa ya kujiajiri wenyewe na kutoa elimu walioipata kwa manufaa ya jamii inayowazunguuka.
 Mkurugenzi wa AQUES LTD TANZANIA NZINGULA M.ZACHARIA AKITOLEA UFAFANUZI WA JAMBO WAKATI WA MAHOJIANO.

Moja ya bwawa ambalo vijana wanaweza kujiajiri kama mmoja wa wahitimu aliyeamua kujiajiri na kuwataka kuiga mfano huo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa