Wednesday, 21 December 2016

AQUES LTD YAZIDI KUJITANUA KIMATAIFA KWA SASA.

Katika kuhakikisha kampuni nguli Tanzania katika utoaji bora wa huduma za miradi ya ufugaji wa samaki hapa nchini,sasa imejipanga kuvusha huduma zake nje ya mipaka ya Tanzania.Akizungumza hayo Mkurugenzi mkuu wa aques ltd Emmanuel Godfrey kuwa kwa sasa Aques inafikiria Zaidi kupanua wigo na kuhudumia nchi mbalimbali duniani kutokana na uzoefu mkubwa walionao kwa sasa na kushirikiana na wataalam nguli kutoka mataifa mbalimbali duniani.

 Mkurugenzi mkuu wa AQUES LTD kushoto akisalimiana na mgeni wake kutoka nchini Norway kuzungumzi jinsi wanavyoweza kufanya kwa pamoja ili kuleta ufanisi wa huduma juu ya miradi ya ufugaji wa samaki kwa sasa.
Aques ni moja ya kampuni amabayo imekuwa ikitoa mchango mkubwa sana kwa jamii kwa kuweka hduma zake kwa njiia ya mtandao buree bila gharama yeyote ile,lakini kwa wale wasio na uwezo wa kupata huduma ya mtandao wanaweza kusoma majarida mbalimbali kama vile mkulima mbunifu na kwenye magezeti likiwemo mwanachi au vipindi vya tv ikiwemo EATV na Star tv,Aques imeomba wadau na wananchi mbalimbali kuwaunga mkono ili kuhakikisha changamoto kadhaa inayoikabili miradi ya ufugaji wa samaki inatatuliwa.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa