Wednesday, 21 December 2016

CHUO KIKUU CHA STIRLINNG KUTOKA UK IMEITEMBELEA KAMPUNI YA AQUES LTD TANZANIA

Maisha mazuri hayataki haraka,wengine wakatungia na nyimbo 'wakisema mdogo mdogo'na ndivyo AQUES LTD wanavyosema baada kupokea mualiko wa kikao maalamu na moja ya wajumbe kutoka chuo kikuu cha Stirling kilichopo UK pia ni wa wajumbe kuoka SARNISSA kuja kuonana na wataalam wa kampuni ya Aques ltd hii ni baada ya kuvutiwa na huduma za kampuni kupitia mitandao huku wakienda mbali na kusema kuwa ni miongoni mwa mitandao inayofanya kazi kwa muda mrefu zaidi ikilezea huduma na utoaji wa mafunzo juu ya miradi ya ufugaji wa samaki hapa nchini.
Kikao hicho kilichoudhuliwa na baadhi tu wataalam wa kampuni hiyo kilichohusu zaidi namna kufanya kwazi pamoja na pia kuona namna kuwafanya utafiti zaidi ili kuwasaidia wafugaji hususani katika upande  wa mbegu na chakula.
Kwa upande wa uongozi wa Aques ltd imefurahi kuona juhudi zaidi ya kampuni yake kuwa inasomwa na watu wamataifa mbalimbali hivyo ni hatua kubwa na amakaribisha watu na wadau mbalimbali waje ili washirikiane pamoja kuhakikisha sekta ya ufugaji wa samki nchi inapiga hatua.
 Kutoka kulia ni mkurugenzi wa AQUES LTD TANZANIA ndg Agnely Lishela,William Leschen kutoka chuo kikuu cha Stirling na anayefuata ni Marie Smedley ,Emmanuel Godfrey na Musa Saidi katika picha ya pamoja.
Kikao kikiendelea kilichofanyika jiji Dar es salaam .

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa