Friday, 16 December 2016

NI WATU WANGAPI WANAFAHAMU SAMAKI ALIYEVULIWA KWA MABOMU?

Ni hoja yangu ya siku ya leo nikiwa mjini tanga na wataalam waliobobea katika masuala mazima ya usimamizi na uthibiti ubora wa samaki hapa jiji Tanga,moja ya mada ambayo ilinigusa kuhususiana na jamii kuhusu ulaji wa samaki ambao wamevuliwa kwa mabomu.
Hakika serikali inafanya juhudi kubwa sana kupambana na uvuvi haramu kwa lengu la kulinda viumbe hai wa sasa na pia kuhakikisha usalama kwa mlaji.
Hivi tuliwashawahi kujiuliza watanzania wangapi wanafahamu samaki aliyevuliwa kwa mabomu?katika mahojiano na watu kadhaa wapo waliosema wanafahamu na baadhi hawafahamu juu ya samaki waliovuliwa kwa mabomu na madhara yake.
Agatha Edward mtaalamu kutoka kitengo cha doria mkoani tanga anaeleza wamekuwa wakiwaelimisha sana kuhusu uelewa wa samaki aliyevuliwa kwa mabomu,anaeleza na kusisitiza sana jamii kuhudhulia kwenye semina mbalimbali ambazo wamekuwa wakizitoa juu ya utambuzi wa samaki walio salama na wasio salama.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa