Sunday, 1 January 2017

HONGERA MH RAIS MSTAAFU J .KIKWETE KWA KUFUNGUA FULSA YA UFUGAJI SAMAKI NA KUFANYA ISIKIKE.Mh Raisi mstaafu Dr J kikwete akisikiliza maelezo kutoka kwa mtaalamu wa ufugaji wa samki nchin Afrika ya kusini.
Hakika harakati za ufugaji samaki zimechangiwa sana na mh wetu raisi mstaafu wa awamu ya nne wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr Jakaya Mrisho Kikwete ,hakika alifungua fulsa hii Zaidi kwa ajili ya kusaidia jamii ya watanzania kufahamu Zaidi juu ya fursa hii ya ufugaji wa samaki hapa nchini kwa lengo la kupunguza umaskini.Alitembelea nchi mbalimbali kujionea wenzetu wanavyofanya miradi hii hakusita kuwaagiza maafisa na wakurugenzi mbalimbali koungeza juhudi Zaidi katika masuala ya ufugaji wa samaki uwe wenye tija Zaidi kwa wananchi wenye vipato vya aina zote.
Kwa sasa ukizungumzia habari ya samaki ni sawa na kusema kuwa NI HABARI YA MJINI kama vijana wa kisasa wanavyosema.
Hakika awamu ya mh mstaafu J kikwete ndiye aliyefanya kuanzishwa kwa mafunzo maalum ya kuwaandaa wataalam wanahusika na masuala ya ukuzaji viumbe maji ambayo kwa ngazi ya cheti hapa nchi ilianza 2010 jambo ambalo mpaka leo limesaidia Zaidi maofisa ugani juu ya miradi ya ufugaji samaki kuwa wengi kutoa huduma hii kwa wakati na kutoa matokeo chanya kwa jamii.
Licha ya changamoto kadhaa kujitokeza kwenye miradi hii lakini juhudi kubwa aliyoifanya Mh Raisi Mstaafu ni kubwa na yakupongezwa Zaidi.
Mtaalamu kutoka nchini Afrika kusini akiwa na mtaalam kutoka kampuni ya AQUES LTD TANZANIA Musa Ngametwa kwa ajili kupata mafunzo maalum ya mradi wa ufugaji wa samaki katika utaalam wa hali ya juu

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa