Tuesday, 21 February 2017

SIO BUSARA KUMTUMIA FUNDI WA KUJENGA NYUMBA AKAJA KUJENGA BWAWA BILA USIMAMIZI WA MTAALAM

Kumekuwepo na mambo mengi sana katika jamii yanayotokea hususani katika miradi hii ya ufugaji wa samaki hapa nchi.Tumepita maeneo mengi sana na kushuhudia baadhi ya wafugaji wa samaki wakilalamika kuvuja kwa mabwawa ya yao.
Moja ya kosa kubwa sana ambalo watu wengi hulifanya ni kutumia mafundi nyumba kujenga mabwawa ya samaki.
Hapa unawezakujiuliza hivi kuna uwiano gani kati ya fundi wa kujenga nyumba na kujenga mabwawa ya kufugia samaki.

Hebu angalia bwawa hili ambalo mojawapo limejengwa na fundi nyumba asiweza kuangalia uwiano na mzigo unaingia ndania yaani maji na samaki wenyewe hali inayopelekea mabwawa mengi kuwa chini ya ubora.

 Huu ni moja wa mfano wa bwawa lililojengwa na wataalam kwa kufuata vigezo vyote muhimu vya ujenzi wa mabwawa ya samaki.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa