Thursday, 16 March 2017

AQUES LTD YATEMBELEA RUVU KUANGALIA HALI YA SOKO LA KAMBALE

 Juhudi kubwa kwa sasa kama kampuni ni kuhakikisha kuwa tunapata soko la uhakika wa bidhaa zinazofugwa na wafugaji lakini pia kuhakikisha ubora wa mazao ya samaki yanayozalishwa.
Mkuu wa kitengo cha Ubora na masoko Masumbuko Nzingula alipotemebelea soko la samaki wa kambale Ruvu darajani na kuzungumza na wauzaji hao ambao wamejikita Zaidi katika soko la samaki aina ya kambale wakavu.
Hakika bado uhitaji wa samaki ni mkubwa samaki kwa jamii ama kwa walaji kwani walaji wa samaki wamekuwa wakiongezeka kila siku hususani watu kuanza kuelewa kuhusu elimu ya lishe bora au ulaji wa nyama nyeupe.
 picha kutoka kulia mkuu wa kitengo cha ubora na masoko kutoka aques ltd akizungumza na muuzaji wa kambale wakavu RUVU DARAJANI.
Moja ya bidhaa za samaki aina ya kambale waliokaushwa vizuri wakiwa tayari kwa ajili ya mauzo.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa