Monday, 20 March 2017

UMUHIMU WA MIZANI KWENYE MRADI WA UFUGAJI BORA WA SAMAKI

Je, huwa una Mizani shambani kwako?

Mizani ni muhimu sana kwenye shamba la ufugaji bora wa samaki na inafaida zifiatazo.

1. Kupima chakula cha Samaki. Usiwe unakisia chakula cha kuwalisha kama unatumia njia ya kulisha kwa uzito.

Fomula ya chakula cha SAMAKI,

Unatakiwa uchukue idadi ya samaki wote waliopo kwenye Bwawa uzidishe wastani wa uzito wa samaki uliwapima kisha uzidishe asilimia ya kiwango chako cha ulishaji (3% - 10%) utapata kiwango cha uzito unaotakiwa kuwalisha samaki wako.

2. Kupima maendeleo ya ukuaji wa Samaki. Samaki wanapaswa kupimwa kila mwezi kujua mabadiliko ya ukuaji wao. Na kwenye kupima sio lazima upime Samaki wote bali una fanya sample ya Samaki na baadae sasa unatafuta wastani wa uzito wao.

3. Kupima uzito wa samaki wote baada ya mavuno.Ni vizuri kupima uzito wa Samaki wako baada ya mavuno ili kufanya ulinganifu wa uzito wa matarajio yako ya mavuno.

Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa namba zifuatazo;

0784 455 683 au 0753 749 992 au 0718 986 328

Au tembelea Face book akaunti yetu: Aquaculture and Environmental Services Ltd. Au website yetu: www.aquestz.com

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa