Friday, 12 May 2017

UMUHIMU WA UHIFADHI WA MAJI KWENYE BWAWA LA SAMAKIØ  Utunzaji wa ubora wa maji ni jambo la msingi katika ufugaji wa samaki kwa kua asilimia kubwa sana samaki hutegemea maji yaliyosafi na salama kwa ajili ya ukuaji wao.Ø  Siri uwezo wa kutambua tabia za maji safi ya kufugia samaki (physical, chemical and biological)

Ø  Uwezo wa kudhibiti ubora wake.

Ø  Utunzaji wa maji ya kufugia samaki

Ø  Maji machafu/maji taka (yasiyo na ubora unaofaa) huathiri afya ya samaki na hata kupelekea kupata magonjwa na kushindwa kukua vizuri.

Ø  Kwa hiyo ni jambo la muhimu sana kuzingatia na kudhibiti ubora wa maji ili kupata mazao mazuri, mengi na kwa wakati  unaotarajiwa.

Ø  Hakikisha kwamba unacho chanzo cha uhakika cha maji.

Ø  Kina cha maji ya bwawa kisiwe chini sana  

Ø  maji yafikie mita 1 kwenye kina kifupi cha bwawa lako.

Ø  rutubisha bwawa ili samaki wapate vyakula vya asili (vimelea maji na viroboto maji),urutubishwaji huo uendane na ukubwa halisi wa bwawa.

Ø  chanzo cha maji kisiwe kichafu -  maji machafu ya majumbani, madawa ya viwandani/ kilimo n.k

Ø  Epuka kujaza maji ya bwawa hadi kwenye kingo za bwawa lako ilikuepuka kufulika kwa bwawa lako na kutoa samaki wako nje ya bwawa

Ø  Weka chujio kwenye mdomo wa bomba la kuigiza maji bwawani au mfereji  ili kuepuka kuingiza viumbe visihitajika kuingia kwenye bwawa.

Ø  kuzuia vyura, na viumbe wengine kuingia kwenye bwawa ili wasije wakawala samaki.

UMUHIMU WA KUTUNZA UBORA WA MAJI KWENYE BWAWA LA SAMAKI

Ø  ukuaji, kuzaana na uhai wa samaki hutegemea ubora wa maji ya kufugia  .

Ø  Maji yenye ubora sahihi huwafanya samaki wakue kwa haraka

Ø  Faida ya ufugaji wa samaki hutegemea ubora wa maji

Ø  Mazao (yields) ya samaki hutegemea ubora wa maji,

Ø  maji machafu hutoa mazao duni na machache. 

MBINU ZA KUTAMBUA UBORA WA MAJI YA BWAWA

Ø  Maji meupe sana – hayana vyakula vya asili - vimelea maji na viroboto maji

Ø  hayo siyo mazuri - samaki hawatakua watadumaa.

Ø  Maji yenye matope – yanaweza kuathiri upumuaji wa samaki  na kusababisha vifo vya samaki

Ø  Maji ya rangi ya kijani sana –vijimelea maji ni vingi.

Ø  Vimelea maji ni chakula lakini vikiongezeka sana husababisha tatizo la upungufu wa  oxigeni

Ø  huweza kuathiri ukuaji wa samaki.

Ø  Samaki wanaogelea sehemu ya juu ya maji

Ø  Inaashiria hakuna oksigeni ya kutosha

MAMBO MUHIMU YANAYOATHIRI UBORA WA MAJI

Ø  Ongezeko la ukuaji wa vimeleamaji

Ø  Kiwango cha chini cha oksigeni ndani ya maji

Ø  Kuwepo kwa sumu zitokanazo samaki na kuozeana kwa vyakula vilivyozidi ndani ya maji (toxic metabolites).

NAMNA YA KUDHIBITI ONGEZEKO LA VIJIMELEA KWENYE BWAWA LAKO.

Ø  punguza maji ya bwawa na kuongeza maji masafi

Ø  punguza kiwango cha chakula au kusimamisha kwa muda ulishaji

Ø  ruhusu samaki wale vijimelea  vilvyoko kwenye bwawa

Ø  acha kurutubisha bwawa kwa muda hadi hali ibadilike

SABABU ZA UPUNGUFU WA OKSJENI NDANI YA MAJI YA SAMAKI

Ø  Kiwango kikubwa cha mbolea huzalisha kwa wingi vijimelea ambavyo huonekana kwwa muonekano wa rangi ya kijani iliyokolea na viroboto maji  (phytoplankton and zooplankton)hutumia oksigeni iliyoko ndani ya maji wakati usiku na wakati mawingu mazito.

Ø  chakula kingi kuliko uwezo wa samaki kukimalaza

Ø  -huzama chini na kuoza na kusabaisha upungufu wa oksigeni ndani ya maji. hewa ya ukaa (corbondioxide), amonia (unionized amonia) hivi vyote huathiri ukuaji wa samaki samaki.

Ø  -Hali ikiendelea hupunguza hamu ya kula, hupunguza ukuaji

Ø  Hupunguza uwezo wa kubadili chakula (food conversion ratio).

Ø  Wingi wa samaki, ikiwa bwawa ni dogo na lina samaki wengi mno huweza kupunguza kwa kiasi kikubwa kumaliza oxygen ndani ya bwawa..

JINSI YA KUTAMBUA KUWA OKSIGENI HAITOSHI KWENYE BWAWA LAKO.

Ø  Tembelea bwawa asubuhi au jioni sana kwenye bwawa lako.

Ø  samaki wakionekana sehemu ya juu ya maji  -  vijimelea ni vingi 

Ø  Zoezi lirudiwe mchana wakati jua likiwa la kutosha.

Ø  tatizo ni bado lipo - inashiria kuwa kuna matatizo zaidi ya vijimelea

Ø  mfano vyakula vinavyooza 

Ø  Kuna  ammonia au kuna hewa ya hydrogen sulfide (toxic metabolites).

Ø  Hutolewa na samaki, bacteria na virobotomaji na vimelea maji (Plankton)

Ø  madhara yake ni makubwa

Ø  Huweza kusababisha vifo

NAMNA YA KUDHIBITI HALI YA UPUNGUFU WA OKSJENI KWENYE BWAWA LAKO.

Ø  Kupunguza maji ya bwawa na kuongeza maji masafi

Ø  Kupunguza kiwango cha chakula mbadala au

Ø  simamisha kwa muda ili kuruhusu samaki wale vijimelea

Ø  simamisha kurutubisha bwawa hadi hali imebadilika.

Ø  changanya maji ya bwawa (wheel paddle)

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa