Wednesday, 13 December 2017

KUNA SABABU ZIPI ZINAZOWAPELEKEA WATANZANIA WAFUGE SAMAKI?.


Historia ya ufugaji wa samaki Tanzania haujawekwa vizuri kwenye maandishi, lakini kulingana na Balarin (1985) anasema majaribio yalianza mnamo mwaka 1949 katika mikoa ya Tanga (Korogwe) na Mwanza (Maly) ikionyesha kujengwa pia kwa mabwawa mengi ya samaki. Lakini mabwawa haya yaliishia kutofanya kazi kwasababu ya kukosa usimamiaji mzuri, matumizi ya technolojia isiyosahihi pamoja na matatizo mengine kama ya ukame na miundo mbinu mibovu
Mwaka 1967 serikali ya Tanzania ilianzisha kampeni ya kuhamasisha ufugaji wa samaki, lakini ilishindikana kwasababu ya mipango mibovu na usimamizi mbovu. Mwaka 1972 kwa mara ya kwanza ufugaji wa samaki ulipewa umuhimu kisera japo sharia ilitungwa mwaka 1970. Mwaka 1997 sera ya ufugaji wa samaki ilipitishwa iliyoipa kipaombele ufugaji wa samaki.
KWA WATANZANIA WAFUGE SAMAKI?.
Kuna upungufu mkubwa sana wa protini duniania na hasa katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania inayotokana kwa asilimia kubwa na vyakula vya aina ya nyama. Upungufu huu wa protini ambayo ni muhimu kwa maendeleo ya kiafya ya binadamu hasa watoto wadogo ambao wanahitaji kukuwa kwa haraka. Ugonjwa wa Kwashako kwa watoto ndiyo matokeo ya upungufu wa protini mwilini.
Pia matumizi ya samaki na hasa mafuta ya samaki ambayo ndo yanatumika sana kuwanywesha watoto wadogo yamethibitika kisayansi kuwa yanasaidia sana ukuaji wa ubongo wa mwanadamu. Lakini pia uwepo wa kiwango kidogo sana cha kolestero ambayo imeripotiwa kusababisha ugonjwa wa moyo kimepelekea ongezeko la watu wanakula samaki.
Sababu zifuatazo hapa chini zinatoa jibu la kwa nini Mtanzania ufuge samaki;
-Ongezeko kubwa la uhitaji wa samaki ndani na nje ya nchi yetu kunakofanya samaki waliopa sasa kutotosheleza mahitaji.
-Kupungua kwa samaki asili kwenye mito, maziwa na bahari kunakotokana na uvuvi wa kupindukia na haramu.
-Urahisi wa kufuga samaki kwa vile hawahitaji eneo kubwa na chakula kisichokuwa na gharama kubwa.
-Wanauwezo wa kutoa mazao mengi (faida kubwa) katika eneo dogo tena ndani ya muda mfupi (uvunaji huanza baada ya miezi mitatu au mine hivi na uvunaji wa mwisho kati ya miezi 6 hadi 12).
-Ufugaji wa samaki utasaidia familia kupata kitoweo pasipo gharama za ziada na tena utapata protini ya uhakika.
-Upatikanaji wa maji maeneo mengi ya nchi yetu hasa angalau kwa muda miezi michache kwa mwaka kiasi cha kutoa fursa ya kuzalisha samaki katika kipindi ambacho maji yanakuwepo. Lakini pia maeneo yenye maji ya bomba yanaweza kuzalisha samaki muda wote wowote.
-Samaki wanavumilia sana magonjwa, hata mazingira duni wanauwezo wa kuishi
-Ardhi tuliyonayo maeneo mengi ya Tanzania inakidhi ufugaji wa samakiTatizo la kuwa kuwa na ufugaji mdogo wa samaki unachangiwa kwa kiasi kikubwa uduni wa elimu ya ufugaji wa samaki katika maeneo mengi. Maeneo ambayo elimu ya kutosha imetolewa watu wengi wamenufaika na ufugaji wa samaki na ufugaji umeshamiri kwa kiasi fulani. Ufugaji wa samaki hauhitaji rasilimali nyingi au zilizo nje ya uwezo wa mwanchi wa kawaida wa Tanzania. Mahitaji ya samaki mengi yanapatikana katika maeneo anayoishi mwananchi na wala hauhitaji muda mwingi kiasi cha kuathiri kazi nyingine.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa