Friday, 29 June 2018

CHANGAMOTO KUBWA TANO ZILIZOWAKUMBA WAFUGAJI SAMAKI.

Ufugaji wa samaki ni kazi ya kupanda,kukuza na kutunza samaki katika bwawa au uzio (uliotengenezwa kwa vyuma,miti pamoja na nyavu) au eneo lolote ambao uthibiti wake uko chini ya mamlaka ya mfugaji mwenyewe.Mabwawa yanaweza yakawa ya kuchimbwa na watu(japo kuwa mabwawa ya asili pia yanaweza kufugia samaki) wakati yale yanaweza yakawekwa katika eneo lolote lenye maji mengi kama vile ya ziwa,mto au bahari.

Ufugaji wa samaki katika kiasi fulani si sawa na ukuaji wa samaki katika mito,maziwa na bahari.Tofauti kubwa iliyopo samaki wanaofugwa na wasiofugwa ipo katika huduma,huduma wanazopata samaki wanaofugwa huwekwa kwa idadi maalumu ndani ya bwawa,kupatiwa chakula na kuhudumiwa vizuri.

Zifuatazo ni baadhi ya changamoto ambazo wameweza kukumbanazo wafugaji samaki

1.MABWAWA KUKUMBWA NA MAJI (MAFURUKO).

Hii ni moja changamoto kubwa sana iliyoweza kutokea katika kipindi cha mwezi wa watatu mpaka wa tano mwaka 2017,mabwawa haya yaliyokumbwa na mafuriko ni moja ya changamoto iliyotokea katika mabwawa ambayo yamechimbwa au kujengwa pasi kufuata taratibu za ujenzi au uchimbaji wa mabwawa,moja ya maeneo yaliyokumbwa na hali hii ni ruvu mkoa wa pwani,morogoro,mwanza,na mtwara hizi ni baadhi ya maeneo ambayo baadhi ya wafugaji wa samaki waliathirika na changamoto hii.

Sababu kuu inayopelekea mabwawa haya kukumbwa na mafurukio ni ujenzi usiozingatia tahadhari za kimazingira ikiwemo watu kujenga mabwawa kandokando ya ziwa,mifereji mikubwa na mabondeni,mara nyingi sana watu huchunguza eneo wakati ambao sio wa mvua hivyo kufikili ni maeneo salama kwao na kuanza kuchimba mabwawa.

Ushauri wa kitaalam kwa wafugaji wa samaki kuchukua tahadhari kubwa kabla ya kuanza ujenzi wa bwawa eneo lazima lifanyiwe uchunguzi wa kutosha kwa wakati wote kiangazi na masika ili kubaini eneo lako kama ni salama au sio salama ili kuepuka hasara zinazoweza kutokea,kuepuka kuchimba kando kando ya vyanzo vikuu vya maji kama vile kujenga bwawa kandokando ya ziwa,mifereji au kwenye mabonde kwani maeneo haya sio salama kwa ajili ya ufugaji wa samaki.

2. TATIZO LA MAADUI WA SAMAKI KAMA VILE NDEGE, KENGE, FISI MAJI NA NYOKA

changamoto hii uwepo wa ndege,kenge na fisi maji hupelekea kwa mfugaji kupata matokeo mabaya asiyoyatarajia kwa sababu samaki hupungua kwa kuliwa na maadui hao,mfano mfugaji anaweza akawa amepanda samaki 1000 hivyo hujikuta wakati wa mavuno samaki wanaopatikana ni 400 kati ya 1000 samaki wengine wameshambuliwa na hao maadui hao.

Sababu  za tatizo hili ni kujenga mabwawa sehemu zenye vichaka au kutovyeka majani kuzunguka bwawa la samaki hushawishi maadui hao kama vile kenge,nyoka na fisi maji huwa ni sehemu yao ya kujificha na baadhi ya mabwawa kutowekwa uzio na wavu wa juu kwa ajili ya kuthibiti maadui hao kupita na kushambulia samaki kirahisi.

Ushauri wa kitaalamu ni kuhakikisha eneo lako linakuwasafi halina kichaka na kuhakikisha kuweka uzio kuzunguka bwawa na kuweka  wavu juu ya bwawa kwa ajili ya kudhibiti ndege kutoingia ndani ya bwawa kirahisi.hivyo kufanya hivyo kunaongeza chachu ya mavuno chanya kwa mfugaji wa samaki.3.UGUMU WA KUKAUSHA MAJI BWAWANI.

Hii ni moja ya changamoto kubwa iliyobainika kwamba wafugaji waliowengi wamechimba mabwawa pasi kuweka mifumo rafiki wa kutolea maji,changamoto au athari kwa kutoweka mifumo ya maji hupelekea ubadilishwaji wa maji kuwa mgumu hali inayosababisha samaki kukaa na maji machafu kwenye mabwawa kwa muda mrefu,madhara makubwa ya maji machafu kukaa kwa muda mrefu kwenye mabwawa hupelekea samaki kukumbwa na magonjwa kama vile fungus au kufanya ukuaji hafifiu sana kwa samaki.

Tatizo hili la ugumu wa utoaji wa maji husababishwa na ujenzi wa mabwawa kutosimamiwa na wataalam husika wa miradii ya ufugaji samaki na mabwawa na pili husababishwa na bwawa

kujenjwa kwenye eneo la tambarare kiasi kuwa hakuna uwezekano wa kutumia bomba au kukata kuta za bwawa kuondoa maji.

Utatuzi wa tatizo hili ni kuhakikisha kuwa unafuata kanuni zote muhimu za uchimbaji wa mabwawa ikiwemo mfumo wa kutolea maji,unachimba bwawa kwa kuzingatia sehemu yenye mwinuko wastani ili kupata mlalo halisi utakao tililisha maji yote kutoka bwawani na kufanya ufugaji mzuri unazingatia kanuni bora za ufugaji samaki wenye tija.4.KUIBUKA KWA UGONJWA WA KUPASUKA KICHWA KWA SAMAKI TATIZO HILO LIMEIBUKA ZAIDI HUSUSANI KWA WAFUGAJI WA KAMBALE.(CRACK HEAD DISEASE IN CATFISH).

Hii ni moja ya changamoto iliyowakumba baadhi ya wafugaji wa samaki kwa msimu uliopita,tatizo hili limelipotiwa na baadhi ya wafugaji hususani wenye mabwawa ya kujengea kwa tofali,baada ya kuona samaki wao wanakufa hususani kambale,kupitia jarida hili la mkulima mbunifu wafugaji kadhaa walioripoti taarifa hizi kwa mtaalam wa samaki alifika na kubaini tatizo hili moja kwamoja kutoka kwa wafugaji,moja ya dalili za ugonjwa huu samaki huanza kwa vilia damu sehemu za juu ya kichwa chake kisha hupasuka na kutengeneza kidonda ambacho huanza kuwa kidogo kisha hukua na baadae hupelekea kifo cha samaki.,

Tatizo hili husababishwa zaidi na ukosefu au upungufu wa baadhi ya virutubisho,moja ya virutubisho hivyo muhimu kwa kambale kuvipata ni vitamin C,uwepo wa vitamin hii humfanya kuimalisha mwili wake na kufanya utengemavu mzuri kwenye mfumo mzima wa mifupa yake,ni hii hutokana sana na ulishaji usiozingatia kanuni bora za utengezaji wa chakula cha samaki kulingana na samaki husika ,hivyo hupelekea kutokea kwa tatizo hilo la kupasuka kwenye sehemu ya mwili wake.

Ushauri wa kitaalam unapoona tatizo hili limetokea haraka sana wacha kutumia chakula ambacho hicho ndio kimepelekea kutokea kwa tatizo hilo,tengeneza chakula au lisha chakula chenye virutubisho vya vitamin C  na amino acid  kwa ajili ya kurejesha hali ya samaki kwenye afya yake,kama tatizo hili litaendelea ni vema sana kupata ushauri wa wataalam wa samaki kwa ushauri wa kina zaidi.

5.WAFUGAJI WENGI KUTOKUWA NA USIMAMIZI MZURI KWENYE MIRADI YAO.

Mradi wowote ili ukue vizuri tunahitaji sana uwepo wa usimamizi mzuri wa mradi huu wa samaki ambao unatija zaidi kwa jamii,moja ya changamoto kubwa sana ambayo imejitokeza zaidi ikiwemo na hii ya usimamizi hafifu kwenye mradi,tunapo sema usimamizi hafifu hapa tuna maanisha kwamba baadhi ya wafugaji wengi wamepata matokeo ambayo sio ya kulidhisha kwenye mavuno yao kwa sababu hakuna uwekaji wa kumbukumbu yeyote ile kuanzia siku ya kuchimba bwawa,kuweka samaki,ulishaji wa samaki na malipo ya vibarua,uwekaji wa kumbukumbu ni moja ya vitu muhimu sana kwenye mradi ambayo itakusaidia wewe kufahamu kuwa umetumia kiasi gani na baada ya mavuno kufahamu umeingiza kiasi gani,baadhi ya wafugaji wamekuwa hawalisha chakula kwa wakati uliopangwa,kutobadilisha maji pindi yanapokuwa yamechafuka,na kutofanya usafi nje ya bwawa hali inayopelekea kukarisha maadui wa samaki kama vile kenge,fisimaji, na nyoka.

Ushauri wa kitaalam ni vema sasa wafugaji kufuata nakuzingatia kanuni zote za ufugaji ikiwemo ulishaji kwa wakati kwa samaki,ubadirishaji wa maji na usafi nje ya bwawa kwa ajili ya usalama ambayo itapelekea kupata matokeo chanya zaidi na kufurahia biashara hii yaufugaji wa samaki.

Hayo ndio changamoto kuu tano zilizowakuta wafugaji wa samaki kwa msimu wa mwaka 2017 hivyo ni vyema sasa mfugaji wa samaki kuzingatia na kuepuka changamoto ambazo zinawezakujitoeza.

0 comments:

Twitter Delicious Facebook Digg Stumbleupon Favorites More

 
Powered by Teknotaarifa